Africa center inakupa shavu la kwenda kujifunza sana nje ya nchi kwa wiki sita.

image

Kila mwaka taasisi ya Africa Centre, huwapa wasanii fursa ya kipee ya kutumia takriban wiki sita hadi nane maalum kwaajili ya kujifunza na kukomaza sanaa wanazofanya.
Mwaka huu kupitia miradi ya ukaazi katika nchi mbalimbali zikiwemo Australia, Brazil, India, Italia, Kenya, Hispania, Tanzania na Marekani, Africa Centre inatoa fursa kwa wasanii takriban 13 kushiriki kwenye mradi wa AIR (Artists In Residency).
AIR inatoa wito kwa wasanii wa Afrika walio na ubunifu, wanaojihusisha na masuala ya jamii na wanaotaka kupeleka sanaa zao nje ya mipaka yao kutuma maombi.
AIR watachagua msanii mmoja kutoka katika wale wataokuwa wameteuliwa na Africa Centre kushiriki kwenye mradi wa ukaazi katika kipindi cha mwaka 2015 au 2016.
Gharama za kuishi, nauli katika mizunguko hiyo na zingine zitagharamiwa kwa wasanii wote watakaoteuliwa kushiriki kwenye mradi huu.
Nafasi hii ipo wazi kwa wasanii wachanga na wakubwa kutoka kwenye fani mbalimbali za sanaa zikiwemo: uandishi, muziki na filamu. Kila nafasi itakuwa na mpangilio wake, matakwa tofauti na muda wake. Kama unataka kutuma maombi katika mradi huu wa ukaazi au kupata taarifa zaidi bofya hapa.
Mwisho wa kutuma maombi ni September, 30, 2015.

Let’s share gud music.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s